The United Church of Canada crest /L'Église Unie du Canada
3250 Bloor St. West, Suite 300
Toronto, ON M8X 2Y4 Canada
Toll-Free: 1-800-268-3781
Fax: 416-231-3103
Website: www.united-church.ca
Loading

The United Church of Canada

Karibu katika Kanisa la Muungano la Kanada!

Trouble reading this page? See our help page!

Tunashukuru ya kwamba uko hapa na twatarajia utapata habari ambayo itakuwa ya muhimu, nay a kukuleta karibu na Mungu.

Historia

Kanisa ya Mungano ya Kanada ni kati ya dini za kiKristo. Ukristo ulianza miaka 2000 liopita na wafuasi wa Yesu. Imeendelea kuwa na kuongezeka kwa karne mingi baada ya kifo kufa na kufufuka kwa Yesu.

Kutoelewana juu ya dini na vitendo kili sababisha kutengana kwa kanisa na kuwa na kanisa tatu ambazo zinapatikana leo. Zote tatu zina pata uamini wawo kutoka na maisha, kifo na wufufuko wa Yesu na wafuasi waake wa zamani. Kanisa katholiki linajitambulisha kuwa wafuasi kupitia kwa Peter, mufuasi wa Yesu na Baba Mtakatifu. Kanisa Katholiki na kanisa la Orthodox waliungana mwanzo wa karne elfu mbili. Katika miaka ya 16th century Pastor Martin Luther nawengineo wenye mafikiro sawa walijitenga kutoka kanisa katholiki na kuwanzisha kanisa la Proestanti ambayo ilisababisha kuwa na makanisa mingi kwa nchi nyingi.

Katika mwaka 1925 makanisa ya vitengo tatu, Methodist, Congregationalist na Presbyterian ya Kanada yaliongana kufanya kanisa la Muungano la Kanada, kupitia kitengo kya Bunge. Maelowano kati ya mula tofauti yanapatikana kwa mula ya historia na motto “wacha wote tuwe pamoja” Ndio sahihi ya Kanisa.

Kutoka mwaka 1925 makanisa mengine madoga ya meungana na kanisa la Muungano la Kanada kwa sasa kuna karibu kanisa 3200 la kanisa la Muungano la Kanada. Hii inaelezea mila na desturi ya kania letu kutoka miaka iliyapita.

Uamini wetu

Kama makanisa mengine ya kikristo kanisa la Muungano la Kanada linafuata. Mafundisho ya Mungu, Yesu na Bibilia. Lakeni namna ambayo tunaelewa Mungu na mafundisho yetu na kusoma Bibilia ni tofauti kama vile ni tofauti kati dini zingine za kikristo. Hapa ni mafundisho na desturi muhimu ya kikristo tunayofuati katika kanisa la Muungano la Kanada.

Tuna sacramenti mbili: ubatizo na communio zote ambazo ni wezo kwa mtu wa umri ye yote. Tunatambua ubatizo kutoka kanisa zingine za kikristo. Kanisa la Muungano la Kanada inafanya kazi pamoja na makanisa mengine ya kikristo wakati iwezekanavyo na kati ya watu wa madini mengine ya dunia kusaida kwa Amani, heshima ya Binadamu.

Misa:

Wafuasi wakiungana Kanisani ni misa.

Inaendeshwa na mufuasi ambaye analipwa na wafuasi wa kanisa. Anapeana uongozi, elimu na maombi. Wafanyika wengine kama mwalimu wa muziki, wafanyikazi wa offisi, na walimu wanajitolea ama kulipwa. Wafanyikazi wanaweza kuwa wanaume ama wanawake, hawajaolewa ama wameolewa. Pesa inayotumika kulipa wafanyikazi natoka kwa sadaka. Sadaka pia inatumika kufanya kazi ya kanisa kote duniani. Ingawa pastor na wafanyakazi wanafukume ya kuongoza kanisa wafuasi na volunteer wanayuku ya kuondelesha kanisa.

Kupata waamini

Unaeza kupata waamini karibu naawe au kutumia website ya kanisa.

Nini Ufanyika Jumapili

Kila kanisa na pastor wanaongoza misa ya Jumapili kutokana na community na mila na desturi zao. Kwa hivyo kunatofauti vile kila kanisa linaendesha  misa yao ingawa kuna mambo ambayo ni sawa.

 • Tunapofika kanisani tunazalimiwa mulangoni na kupewa mpangalio wa misa. Hu inatueleza mambo ambayo yatafanyika kanisani sikuhivyo na wiki nzima.
 • Watoto wanakaa na wazazi wao misa inapoanza na baadaye wanachukuluwa na mwalimu wa shule ya kanisa.
 • Kwa wazazi wenye watoto wadogo tuna nursery na mtu ambaye atalinda watoto lakini ukitaka kulea mtoto wako ni sawa.
 • Misa ni saa moja.
 • Kuna masomo kutoka Bibilia na maandiko mengine.
 • Kanisa la Muungano la Kristo tunapenda kuimba. Muziki na maneno yanapeanwa kwa karatasi ama kutoka kwa kitabu cha nyimbo.
 • Pastor ama mtu mwingine anapeana mahubiri ambayo inafuata na somo la Bibilia, maisha, na mabo yanayofanyika duniani.
 • Kuna maombi mengi wakati wa misa. ZIngine zinapeanwa na pastor na wafuasi wengine Kanisa la Muungano watu husali wakuwa wameketi sio kupiga magoti.
 • Communio inapeanwa mara nyingi kwa mwaka lakini sio kila jumapili. Iko wazi kwa wote waliokanisani lakini si lazima.
 • Sadaka kwa njia ya pesa huchukulwa ili kusaidia kulipa pastor na kazi ya kanisa kote duniani.
 • Baada ya misa watu wanakutana kwa vinywaji na maongeo.

Maisha ya Kanisa kwa wiki

Jumuia na urafiki ni muhimu kwa kanisa. Ibada nyingi na vitendo yetu vina kuezesha kuungana na kukutana na watu wengi. Inakusaidia kufanya urafiki na vitu via maana.

 • Chakula cha mchana na jioni kwa wafuasi
 • Kujijenga kiroho na urafiki
 • Upishi wa chakula ya kupelekea wazee
 • Usaidize wakati wa shida  kama ugonjwa, kito
 • Chama cha vitabu
 • Kikundi cha wamama
 • Kikundi cha wanaume
 • Masomo ya Bibilia
 • Usaidize kwa wazazi wapya
 • Kwaya ya watoto na watu wazima
 • Michezo ya kuigiza
 • Kushona na useremala
 • Vikunzi vya vijana
 • Masomo na Menginavyo
 • Usaidize kwa chakula na nguo

Kwa hivyo kuna njia nyingi za kuyiunga. Labela unamaarifa Fulani ambayo itasaidia kujenga kanisa la Muungano ka Kanada. Karibu. www.wondercafe.ca

Last updated:
2007/05/21
Created:
2007/05/21