The United Church of Canada/L'Église Unie du CanadaTrouble reading this page? See our help page!
Kanisa la Muungano la Canada ndilo Kanisa kuu la kiprotestanti katika Kanada. Twawahudumiya zaidi ya watu milioni tatu katika makanisa 3677 katika Kanada. Yetu ni historia tajiri ambayo inalinganishwa na maendeleo ya nchi la Kanada.
Kanisa la Muungano la Kanada iligunduliwa kikamilifu katika mwezi Juni, tarehe 10, mwaka 1925 katika mji wa Toronto, Ontario, wakati Kanisa la kimetodisti, Kanada, na makanisa 70 juu ya 100 ya wa presbiteri walijiunga katika mahuluku ya umoja. Waliwo jiunga pia walikuwa kikundi ndogo cha Baraza Kuu la umoja wa makanisa, ambao lililokuwa katika upande wa magharibi wa Kanada. Hii ndiyo ilikuwa muungano wa kwanza wa makanisa duniani ku vuka laini ya majina kihistoriya na kupokea mradi wa sifa kati ya mataifa. Kichocheo kwa ajili ya umoja kilijitokeza kwaajili ya kuhudumia upande kuu wa kaskazini wa kanada na kwa katika haja ya ujumbe wa n’gambo. Kila moja wa kanisa lenyi kujiunga ilikuwa na historiya kabla ya 1925.
Mufaransa Huguenots, akitoroka masumbufo kufwatana na tanguo la “Edict of Nantes”, alileta Imani Ongofu Kanada. Lakini, hata katika ardhi Mpya, maendeleo na nafuu yao ilikuwa pungufu. Baada ya kutowa Novo Scotia kwa Uingereza katika mwaka wa 1713, wageni wa wapresbiteri
kutoka kutoka Scotland na Ireland wakatopea kundi ndogo la wa wafaransa. Makasisi wa kwanza kutoka Scotland walikuwa Daniel Cook, David Smith na Hugh Graham ambao walipanga upresbiteri ya Turo katika mwaka 1786. Katika mwaka 1795, hii presbiteri ilijiunga na ingine, presbiteri ya Pictou, ambao iliwakilisha ingine mtengano ya upresbiteri kutoka Scotland. Katika mwaka 1817, hizi vipande mbili zilijiunga na kuunga Synodi ya Kanisa la Presbiteri la Novo Scotia.
Kufwatana na dharura la ambazo zili sukuma uundaji wa Sinodi ya Novo Scotia, wa presbiteri walisonga upande wa katikati na mangaribi ya Kanada. Kuhusu upande wa mashariki,walileta vipande tafauti za kanisa la Scotland na kuunga wapresbiteri kadha na sinodi , yakwanza ikiwa Upresbiteri wa Kanada munamo mwaka 1818. Kuanzishwa kwa mabuuni ya sinodi mpya iliendelea katika mwaka karne ya kumi na tisa, kwa sehemu ndogo kwa ajili ya ku ingizwa kwa mgawanyiko katika Kanisa la Scotland, ku fika kwa wagenyi wasioongea kingereza ( Dutch Reformed), na kufunguliwa kwa bara mpya unpande wa mangaribi. Kifikiya kati ya karne, mwelekeo ukanza ku badilika, na katika mwaka wa 1875, mafuatano ya dharura ikaamrisha umoja ya wengi wa wapresbiteri katika Kanisa la Presbiteri la Kanada.
Umetodisti katika Kanada ume chapwa na Lawrence Coughlan, Muhubiri Mwayalandi wa kimetodisti amabae alikuja Newfoundland katika mwaka 1765. Alipo rudi Uingereza, wengi wa watu alio rakabisha wakatamka kwa wazi kwamba niwa metodisti .
Huko nyuma, wa metodisti walikuwa wakihama kutoka Uingereza kueleka Novo Scotia; kati yao kulikuwa William Black, Sr. Katika mwaka wa 1779, uamusho kati yao ukapeleka uongofu wa William Black, Jr, wakati huo lakini alikuwa na myaka 19. Akaanza ku hubiri, kuwatembelea makao jirani, na katika mwaka 1781 akasafiri kati ya mji wote wa Nova Scotia ku awadha masomo ya kimetodisti. Kazi yake ikipanua baadaya myaka mbili wakati wahamaji waliwokuwa waminifu kwa Uingereza walihamiya Nova Scotia baada ya mageuzi ya America. Katika mwaka wa 1784, Black alisafiriya Baltimore,Marylanda, kwa ajili ya mkutano ambao ulisafidhisha Kanisa mpya la Metodisti Episcopal. Kazi la kikanada ambalo Black endeleza ilichuliwa chini ya uwangalishaji wake. Kazi ya Kanada iliendelea kama sehemu ya kanisa Metodisti Episcpal mpaka mwaka 1828 wakati ilijitenga na kuwa huru.
Huko nyuma, wametodisti kutoka Uingereza walihamiya Kanada, na kama wa metodisti kutoka Scotland, walileta magawanyiko mbalimbali ya wametodisti wa uingereza. Umoja katika mwaka wa 1874 na 1884 ni matokeo ya Kanisa la metodisti, Kanada ikiwa ime umbwa.
Ushirika mjini Kanada ulitokana na kukubaliwa kwa toleo lililo fanywa na serekali ya Uingereza ambao ili toa ahadi ya kuwapa ardhi ya bure kwa wangereza wenyi kuhamiya Nova Scotia. Katika mwaka 1759, wahamaji wengi wakajenga miji mpya na makanisa; ya kwanza ikiwa hapo Chester, na katika mwaka 1761 kanisa liliumbwa. Katika mwaka 1760, koloni lili anza katika Maugerville, New Brunswick, na kanisa la kwanza likaanza mika sita badae. Kanisa la kwanza mjini Newfoundland lili anza katika mwaka wa 1846. Katika mwaka wa 1801, makanisa za wangereza wakapeleka misioni kuanzisha kanisa katika mji wa Quebec.
Quebec, ambao ilijitokeza na kikundi cha zamani zaidi katika mwaka 1906. Umoja wamakanisa mpya ambao ilipata Mkutano ya Ontario ya “American-based United Brethren in Christ” katika mwaka wa 1907.
Mshiriki mkuu katika umoja mwaka 1925, Baraza kuu la Umoja wa Makanisa ya Mangaribi ya Kanada, ilikuwa mtoto ya azimio ya zamani ya umoja ambao ili kuwa kisukumizi ya kundwa kwa Kanisa la Muungano la Kanada. Hawala ya azimio ya Umoja ili tolewa katika mwka wa 1908. Katika mwezi wa Novemba ya mwaka hiyo, kanisa mpya ikajitokeza katika mji wa Saskatchewan ambao ilikubali azimio iliyo tolewa kama msingi ya shirika. Baadae, wengini wakafwata. Katika mwaka wa 1912, makanisa mengi ya kienyeji wangajiunga na kuunda Baraza Kuu kwaajili yaku shikiliya maswali ya kawaida (baadhi yao ikiwa ya kisheriya), na ku harakisha azimio ya muungano.
Umoja katika mwaka 1925 ulikuwa sauti yenyi kusika. Karibu ya watu 30 juu ya 100 ya wapresbiteri walikataa kuingia umoja nawakabaki kama wa presbiteri.
Kwakufikia kusudio yao yakuwa kanisa lenyi kuunga, kanisa la muungano imetajirishwa na miungano mbalimbali kutoka mwaka wa 1925. Baraza kuu la 4 la Kanisa la Muungano la Kanada (1930) limekubali umoja wa Synodi ya Wesleyan Metodist Church of Bermuda na Kanisa la Muungano la Kanada kwa sharti kwamba sinodi lazima ijishugulishe kama presbiteri ya Maritime Conference pasipo kuingiliya haki na uwezo uliwo pewa na sheriya ya Bermuda katika Wesleyan Methodist Church Act, 130. Baraza la 22 la Kanisa la Muungano la Kanada (1966) lilikubali Mpango wa Umoja wakati “Canada Conference Evengical United Brethren iligueka kuwa moja wa Kanisa la Muungano la Kanada, kuanza tarehe 1 Januari, 1968.
Zaidi ya hayo, wakati zikipita makanisa mbalimbali kutoka vituo tafauti vya kikristo walijiunga na Kanisa la Muungano. Katika mwaka wa 1943, zaidi ya milolongo mbili ya mabidiliano na kanisa la Kianglikani la Kanada ikaanzishwa. Baadae, Kanisa la kikristo ( Wafwasi wa Kristo) wakajiunga kwa mabadiliano Agizo kuu linalo wakilisha makanisa tatu wakachukuwa Azimio ya Umoja katika mwaka wa 1972, lakini miaka tatu baadae ikakataliwa na Kanisa la Kianglikani la Kanada. Mashauriano na kanisa la kikristo ikakamilishwa katika mwaka wa 1985.
Karibuni, Kanisa la Kianglikani la Kanada na Kanisa la Muungano la Kanada walianzisha maongezi. Hii ndiyo maongezi ya kwanza kufanyika rasmi tangu mwisho wa azimio ya maongezi kati ya madhehebu hizo mbili kuhusu mpango wa maongezi ya Umoja munamo mwaka wa 1970.