The United Church of Canada crest /L'Église Unie du Canada
3250 Bloor St. West, Suite 300
Toronto, ON M8X 2Y4 Canada
Toll-Free: 1-800-268-3781
Fax: 416-231-3103
Website: www.united-church.ca
Loading
Quick Links

Overview

Msingi wa Muungano

Trouble reading this page? See our help page!

Kama ilivyotayarishwa na kamati ya pamoja ya Kanisa la Kipresibiteri la Kanada, Kanisa la Kimethodisti, na Makanisa ya Kiusharika ya Kanada, na kupitishwa na Mahakama Kuu za makanisa haya, kama ilivyorekebishwa na Kanisa la Muungano la Kanada.

Jumla

1.1

Jina la Kanisa lililoundwa na muungano wa Wapresibiteri, Wamethodisti, na Makanisa ya Kiusharika ya Kanada litakuwa “Kanisa la Muungano la Kanada”.

1.2

Itakuwa sera ya Kanisa la Muungano kuendeleza roho ya umoja kwa matumaini kwamba haya mawazo ya umoja, kwa wakati uliokubalika, kuhusiana na Kanada, yatachukua sura katika kanisa ambayo itaelezeka kihalisi kama ya kitaifa.

Mafundisho

2.0

Sisi, wawakilishi wa Wapresibiteri, Wamethodisti na matawi ya makanisa ya Kiusharika ya Kanisa la Kristo Kanada, tunatamka hapa kiini cha imani ya Kikristo, kama ilivyo miongoni mwetu. Kwa kufanya hivyo, tunajenga juu ya msingi uliowekwa na mitume na manabii, Yesu Kristo Mwenyewe akiwa jiwe kuu la pembeni. Tunadhibitisha imani yetu katika Maandiko ya Agano la Kale na Jipya kama chimbuko kuu na kiwango cha msingi cha imani na maisha ya Kikristo. Tunakubali mafundisho ya kanuni kuu za imani za Kanisa la mwanzo. Zaidi ya hapo tunadumisha utii kwa mafundisho ya kiinjili ya mageuzi, kama yalivyotolewa kwa pamoja katika viwango vya mafundisho yaliyokubaliwa na Kanisa la Kipresibiteri la Kanada, Umoja wa Kiusharika wa Ontario na Quebec, na Kanisa la Kimethodisti. Tunawasilisha kauli ambata kama muktasari mfupi wa imani yetu ya pamoja na kuipendekeza kwa uangalifu wa makini wa wanachama na wahumini wa makanisa yaliyo katika majadiliano, kama kiini kinachoweza kukubalika kwenye mafundisho ya Maandiko Matakatifu.

2.1 Ibara ya I. Ya Mungu

Tunaamini katika Mungu mmoja tu wa kweli anayeishi, Roho, wa milele, hasiyebadilika, katika uwepo wake na ukamilifu; Bwana Mwenyezi, ambaye ni upendo, mwenye haki katika njia zake zote, mwenye utukufu katika utakatifu, mwenye hekima isiyochunguzika, mwenye rehema nyingi, aliyejaa huruma, mwenye wema na ukweli tele. Tunamuabudu Yeye katika umoja wa Mungu Baba na muujiza wa Utatu Mtakatifu, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, nafsi tatu zenye kiini kimoja, sawa katika nguvu na utukufu.

2.2 Ibara ya II. Ya Ufunuo

Tunaamini kwamba Mungu amejifunua Yeye Mwenyewe katika asili, historia, moyo wa mtu; kwamba kwa neema amependezwa kujifunua mwenyewe kwa watu wa Mungu ambao waliongea walipoguswa na Roho Mtakatifu; na katika utimilifu wa wakati amejifunua kihalisi katika Yesu Kristo, Neno lililofanyika mwili, ambaye ni nuru ya utukufu wa Baba na sura ya nafsi Yake. Tunapokea Maandiko Matakatifu ya Agano la Kale na Jipya, yaliyoandikwa kwa msukumo wa Mungu, yaliyo na utawala wa imani na maisha yasiyoshindwa, kumbukumbu ya uaminifu wa ufunuo wa neema ya Mungu, na yaliyo ushuhuda kwa kweli wa Kristo.

2.3 Ibara ya III. Ya Makusudi ya Kiungu

Tunaamini kuwa makusudi Mungu ya milele, busara, takatifu, na yenye upendo yanajumuisha matukio yote ambayo, wakati uhuru wa mtu hauchukuliwi, wala Mungu sie aliyeweka dhambi, bado katika majaaliwa Yake hufanya vitu vyote kufanya kazi kwa pamoja katika utimilifu wa usanifu wake wenye enzi na utukufu wake.

2.4 Ibara ya IV Ya Uumbaji na Mamlaka

Tunaamini kuwa Mungu ni muumbaji, mtetezi na mtawala wa vitu vyote; kwamba yuko juu na ndani ya kazi yake yote; na amemuumba mtu kwa mfano wake, kukutana na kuwa na ushirika naye, kuwa huru na kuweza kuchagua jema na baya and kuwajibika kwa Muumba na Bwana.

2.5 Ibara ya V. Ya Dhambi ya Mwanadamu

Tunaamini kuwa wazazi wetu wa kwanza, walijaribiwa, wakachagua baya, hivyo wakawa mbali na Mungu na wakawa chini ya nguvu ya dhambi, adhabu ambayo ni ya kifo cha milele; na kwamba, kwa sababu ya kutotii huku, wanadamu wote wanazaliwa na dhambi ya asili, kwamba tumevunja amri ya Mungu na kwamba hakuna atakayeokoka bali kwa neema Yake.

2.6 Ibara ya VI. Ya Neema ya Mungu

Tunaamini kuwa Mungu, kwa upendo wake mkubwa kwa dunia, alimtoa Mwanae pekee kuwa Mwokozi wa wenye dhambi, na katika Injili inayotoka bure wokovu kamili kwa watu wote. Tunaamini pia kwamba Mungu, katika furaha yake njema, alimpa mwanae umati mkubwa wa watu, waliochaguliwa katika Kristo kuingia kwenye utakatifu, huduma na wokovu.

2.7 Ibara ya VII. Ya Bwana Yesu Kristo

Tunaamini katika na kumkiri Bwana Yesu Kristo, mpatanishi pekee kati ya Mungu na mwanadamu, ambaye akiwa Mwana wa Milele wa Mungu, kwa ajili yetu wanadamu na kwa wokovu wetu alijifanya mtu kweli, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na akazaliwa na Bikira Maria, bila dhambi. Kwetu sisi ametufunulia Baba, kwa Neno lake na Roho, aliyaweka bayana mapenzi halisi ya Mungu. Kwa ukombozi wetu, alikamilisha haki zote, alijitoa sadaka kamili msalabani, akatimiza haki za kiungu, na kuichukua dhambi ya dunia nzima. Alifufuka toka kwa wafu na kupaa mbinguni, ambapo daima anatuombea. Adumu milele katika mioyo ya waumini kama Kristo mkazi; anatawala juu yetu ; kwa sababu hii tunampenda, tunamtii na kumwabudu kama Mtume, Kuhani na Mfalme.

2.8 Ibara ya VIII. Ya Roho Mtakatifu

Tunaamini katika Roho Mtakatifu, Bwana na Mtoa Uzima, atokaye kwa Baba na Mwana, atembeaye juu ya mioyo ya wanadamu kuwakinga na dhambi na kuwashawishi katika mema, na Baba yake yuko tayari siku zote kuwa wale wote wanaomwomba. Tunaamini kwamba amenena kupitia kwa watu watakatifu wa Mungu katika kufanya ukweli wake ujulikane kwa wanadamu kwa wokovu wao; kwamba, kwa njia ya Mwokozi wetu aliyetukuka, alitumwa kwa nguvu kuitia hatiani dunia yenye dhambi, kuziweka nuru dhamira za wanadamu katika ufahamu wa Kristo, na kuwashawishi na kuwawezesha watii wito wa Injili; na kwamba anaishi na Kanisa, anaishi katika kila muumini kama roho wa kweli, wa nguvu, wa utakatifu, wa faraja na wa upendo.

2.9 Ibara ya IX. Ya Wongofu

Tunaamini katika haja ya wongofu, ambapo tunafanyika viumbe vipya katika Kristo Yesu kwa njia ya Roho wa Mungu, ambaye anatupa uzima wa kiroho kwa neema na muujiza wa utendaji wa nguvu zake, kwa kutumia njia za kawaida ukweli wa neno lake na sheria za wadhifa wa kiungu katika njia zinazokubalika katika asili ya mwanadamu.

2.10 Ibara ya X. Ya Imani na Toba

Tunaamini kwamba imani katika Kristo ni neema iokoayo tunapompokea, tunapomwamini na kupumzika kwake pekee kwa wokovu kwa maana alitolewa kwetu katika Injili, na kwamba hii imani iokoayo daima inaambatana na toba, ambamo tunakiri na kuacha dhambi kwa dhumuni kamili la kumtii Mungu katika upya.

2.11 Ibara ya XI Ya Haki na Uana

Tunaamini kwamba Mungu, kwa msingi halisi wa utii kamili na sadaka ya Kristo, anawasamehe wale ambao kwa imani wanampokea kama Mwokozi na Bwana wao, anawakubali kama wenye haki, na anawakirimu haki ya kuwa watoto wake, kwa haki ya heshima zote zinazistahili, ikiwa ni pamoja na uhakikisho wa uana wao.

2.12 Ibara ya XII. Ya Utakaso

Tunaamini kwamba wale walioongoka na kupewa haki wanakua na kufananishwa na Kristo katika ushirika pamoja naye, wakiwa na Roho Mtakatifu mioyoni mwao, na utii wa ukweli; kwamba maisha matakatifu ni tunda na ushaidi wa imani inauyookoa; na kwamba tumaini la muumini la kuendelea katika maisha haya ni katika neema ya Mungu inayohifadhi. Na tunaamini kwamba katika kukua huku katika neema wakristo wanaweza kufikia ukomavu na uhakika kamili wa imani ambapo upendo wa Mungu unakamilika ndani yetu.

2.13 Ibara ya XIII. Ya Maombi

Tunaamini kwamba tunatiwa moyo kumkaribia Mungu, Baba yetu aliye Mbinguni, katika jina la Mwanae, Yesu Kristo, na kwa niaba yetu wenyewe na ya wengine kuitoa mioyo yetu kwa unyenyekevu lakini huru mbele yake, tukiwa watoto wake wapendwa, tukimpa yeye heshima na sifa kwa ajili ya jina lake takatifu, tukimwomba yeye ajitukuze duniani kama ilivyo mbinguni, tukikiri dhambi zetu mbele yake na tukimshukuru yeye kwa kila zawadi ya mahitaji katika maisha haya na kwa wokovu wa milele. Tunaamini pia kuwa, kadri Roho Mtakatifu anavyoelekeza jinsi kufanya maombi yote, kwa kujibu atatutunukia kila baraka kufuatana hekima yake isiyochunguzika na utajiri wa neema yake katika Yesu Kristo.

2.14 Ibara ya XIV Ya Sheria ya Mungu

Tunakiri kwamba sheria adilifu ya Mungu, iliyofupishwa katika Amri Kumi, iliyoshuhudiwa na mitume na kufunuliwa katika maisha na mafundisho ya Yesu Kristo, inasimama milele katika ukweli na haki, na haikufanywa kwa imani tupu, lakini kinyume chake iko imara. Tunaamini kwamba Mungu anamtazamia kila mtu kutenda matendo mema, kupenda rehema, na kutembea kwa unyenyekevu na Mungu; na kwamba ni katika upatanisho huu na kwa mapenzi ya Mungu yatatimizwa kwamba katika undugu wa mwanadamu Ufalme wa Mungu utadhihirika.

2.15 Ibara ya XV. Ya Kanisa

Tunakiri Kanisa moja takatifu Katoliki, ushirika wa idadi isiyohesabika ya watakatifu wa kila umri na taifa, ambao wanaunganishwa na Roho Mtakatifu kwa Kristo Kichwa chao ni mwili mmoja katika yeye na wana ushirika na Bwana wao na kati yao. Zaidi ya hapo, tunalipokea hili kama mapenzi ya Kristo, kwamba Kanisa lake duniani litakuwepo kama undugu bayana na takatifu, likijumuisha wale wanaoikiri imani katika Yesu Kristo na utiifu kwake, pamoja na wototo wao, na watoto wengine waliobatizwa, na kuandaliwa kulikiri jina lake, kwa ibada ya umma kwa Mungu, kwa usimamiaji wa sakramenti, kwa kuwaimarisha watakatifu, na kwa uenezaji wa jumla wa Injili; na tunakiri kwa sehemu, kwa wingi au uchache wa usafi, undugu wa ujumla, kila kanisa duniani kote ambalo likaikiri imani katika Yesu Kristo na utii kwake kama Bwana na Mwokozi wa kiungu.

2.16 Ibara ya XVI. Ya Sakramenti

Tunakiri kuwepo sakramenti mbili, Ubatizo na Meza ya Bwana, ambazo zilisimikwa na Kristo, ziwe wajibu wa kudumu kama alama na mihuri ya agano lililoidhinishwa na damu yake ya thamani, kama njia ya neema, ambayo, ikifanya kazi ndani yetu, haitatuharakisha tu bali pia kututia nguvu na kuifariji imani yetu katika yeye, na kama kanuni ambapo kushika desturi za Kanisa lake ni kumkiri Bwana wake ikitofautishwa bayana na sehemu baki ya ulimwengu.

2.16.1 Ubatizo kwa maji katika jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu ni sakramenti inayoonyesha umuhimu na kuweka chapa muungano wetu na Kristo na kushiriki kwetu katika baraka za mapatano mapya. Wahusika halisi wa ubatizo ni waumini na watoto wadogo wakiwakilishwa na wazazi au wasimamizi katika imani ya kikristo. Wazazi au wasimamizi wawafunze watoto wao katika malezi na maonyo ya Bwana na wategemee kuwa watoto, kwa kazi ya Roho Mtakatifu, watapokea faida za sakramenti. Kanisa linawajibika sana kuwapa mafundisho wa kikristo.

 2.16.2 Meza ya Bwana ni sakramenti ya komunyo pamoja na Kristo na watu wake, ambapo mkate na divai vinatolewa na kupokelewa kwa shukrani katika kumbumbuka yeye na kujitoa kwake msalabani; na wale wanaopokea katika imani vile vile katika roho wanashiriki mwili na damu ya Bwana Yesu Kristo kwa furaha , afya na kukua katika neema. Wote wanaweza kuruhusiwa kushiriki meza ya Bwana, ambao wanakiri kikweli kweli imani yao katika Bwana Yesu na utii wa sheria yake.

2.17 Ibara ya XVII. Ya Utumishi

Tunaamini kwamba Yesu Kristo, kama Mkuu wa Kanisa, ameteua humo Utumishi wa Kichungaji katika Neno, Sakramenti, na Uchungaji na Utumishi wa Udiakonia katika Elimu, na Uchungaji na anatoa wito kwa wanaume na wanawake kushiriki huduma hizi; na kwamba Kanisa, chini ya uangalizi wa Roho Mtakatifu, linawatambua na kuwachagua wale wanaitwa, na litawasimika kwa kazi ya Mungu.

2.18 Ibara ya XVIII. Ya Mpango na Ushirika wa Kanisa

Tunaamini kwamba Mkuu na Kichwa pekee cha Kanisa ni Bwana Yesu Kristo; kwamba ibada yake, mafundisho, nidhamu, na utawala yabidi viendeshwe kadri ya mapenzi yake na watu waliochaguliwa kwa ubora wao na kuacha ofisi zao; na kwamba japokuwa Kanisa linaloonekana linaweza kuwa na watu wasio bora na makosa yanaweza kufanyika, lakini waumini hawatakiwi kuwatenga tu kutoka kwenye usharika, bali waishi pamoja nao kwa undugu, ushirika utolewe, kama Mungu anavyotoa nafasi hiyo, kwa wote kila mahali kuliitia jina la Bwana Yesu.

2.19 Ibara ya XIX Ya Ufufuo, Hukumu ya Mwisho, na Maisha ya Baadaye

Tunaamini kuwa kutakuwepo ufufuo wa wafu, wa wenye haki na wasio haki, kwa nguvu ya Mwana wa Mungu, ambaye atakuja kuwahukumu walio hai na wafu; kwamba mwishowe wasiotubu watapotelea katika adhabu ya milele na wenye haki kwenye uzima wa milele.

2.20 Ibara ya XX Ya Huduma ya Kikristo na Ushindi wa Mwisho

Tunaamini kwamba ni jukumu letu, kama wanafunzi na watumishi wa Kristo, kuendeleza Utawala wake hapa duniani, kufanya mema kwa watu wote, kudumisha ibada ya pamoja na ya binafsi kwa Mungu, kuitukuza Siku ya Bwana, kuhifadhi ndoa na utakatifu wa familia, kutii mamlaka ya serikali, na hivyo kuishi kwa uaminifu, usafi na moyo wa utoaji, kwamba maisha yetu yamshuhudie Kristo. Kwa furaha tunalipokea neno la Kristo, tukiwataka watu wake kwenda duniani kote na kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi, kuwatangazia kwamba Mungu alikuwa katika Kristo kuipatanisha dunia na yeye, na kwamba watu wote waokoke na kuifahamu kweli. Kwa ujasiri tunaamini kwamba kwa nguvu na neema zake maadui wake wote mwishowe watashindwa, na ufalme wa dunia hii utafanywa kuwa Ufalme wa Mungu wetu na wa Kristo wake.

Last updated:
2007/05/23
Created:
2007/05/23