The United Church of Canada crest /L'Église Unie du Canada
3250 Bloor St. West, Suite 300
Toronto, ON M8X 2Y4 Canada
Toll-Free: 1-800-268-3781
Fax: 416-231-3103
Website: www.united-church.ca
Quick Links
  • Text Size: A A A
  • Print This Page
  • Share/Save

Beliefs

Muhtasari wa Kanisa la Muungano la Kanada

Trouble reading this page? See our help page!

Biblia

Biblia ni ya maana sana kwa Kanisa la Muungano la Kanada. Kama chanzo ya hekima, ombi la kibinafsi, na stahamini, na twa amini kwamba Biblia inawaza tukaribisha na Mungu.
Biblia yabaki moja ya njia nzuri yenyi kujaribu kuendeleza kazi yauumbaji na uokovu katika dunia, ikitupea msamaha, uponaji, na maisha mpia katika Yesu.

Mara nyingi twarejelea kwakifungo kama “neno la Mungu”.Kwa hii twamaanisha mwandishi alipewa mwangaza ya Mungu.
Pia twajuwa kwamba vitabu mbalimbali ambavio vimeunda Biblia ni hadithi ya jamii mbili za zamani zilizo jaribu kuwa waminifu kwa Mungu katika hali gumu- Israeli ya Zamani na msukosuko wa Wakristu wa kwanza.Kwamfano, hatusamehe utumwa,ama kuwatupiya mawe waliwo tenda uashereti.Pamoja na hayo, katika simulizi zake na mafundisho zake, Biblia ina maneno ya kilinge ya nguvu yenyi kuelimisha.

Sakramenta

Sakramenta ni tendo ya kiroho-udhahiri wa Imani yetu. Kanisa la Muungano lina

sakramenta mbili :Ubatizo na Komonio. Hizi ndizo zalazima sana kwa imani yetu.

 

Ubatizo

Ubatizo ni tendo lenye kumaanisha maisha mpya ambao Mungu anatupea wakati tunajiunga na jamii ya kanisa.
Ubatizo yatumiya maji kama alama yakusafisha ambao inamaanisha kukubali maisha mpya katika kanisa. Sakramenta ya ubatizo ni adhimisho ya kipekee ya jando katika jamii ya kikristo ambao ni kanisa.

Kanisa la Muungano la toa ubatizo kwa watu wa miaka yote.Twaamini kwamba kipaji cha upendo wa Mungu haulinganishwe na uwezo wetu wakuielewa, kwahiyo twawabatiza watu wakiwa watoto hata wale wakubwa.

Kwa watoto, mafundisho ya tolewa kwa wazazi ama kwa wadhamini wao, kwaajili wawalee katika hali ya kikristo. Wakati wa sherehe, kila moja katika kanisa atoa agano ya kuwaunga mkono mtoto na/ ama wazazi wake.

Ubatizo siyo hitaji kwa kupata upendo wa Mungu.Twaamini kwamba watu waliwo kufa bila ubatizo hawako katika hukumu, ama hawajapotea; wala kulaaniwa.
Ubatizo katika kanisa la Muungano imetambuliwa na makanisa zote ambazo zakubali ubatizo wa watoto. Kadhalika, ikiwa mtu amebatizwa katika kanisa lingine, kanisa la Muungano lautambua ubatizo wao na wakaribishwa kama wakristo.

Ukomonio

Ukomonio ni alama ya chakula amabao inawakarisbisha watu wote. Niukumbusho wa karamu ya mwisho ya Yesu pamoja na wafwasi wake na inaendelea kama alama ya upendo wa Mungu unao dumu.

Uingianaji

Yesu aliwakaribisha watu wote, wakiwa maskini, tajiri, ama wakipita; wagonjwa kama wazima; wenye elimu na wasiwo kuwa na elimu, wenye kupendeza na watenga, wathabiti na wenye kujaa shaka.
Kanisa la Muungano inajivunia kuwakaribisha watu wote jinsi Yesu alifanya, pasipo kuangaliya miaka, kabila, hali, jinsia, mwelekeo, ama uwezo wa kimwili.

Watoto

Kanisa la Muungano latumika kwa bidii kwakuwakubali watu wa miaka yote, tangu wa babu hadi watoto wachanga.

Watoto hawaonekane kama watuwazima wenye kungoja, ama kama wenyi kwafurahisha watu wazima. Wamekubaliwa kwaukweli na wamekaribishwa kama washirika katikati ya kila kanisa, wakileta mawazo na mawaidha na vipawa via kipekee ambao inaweza kuangaziya kanisa nzima.

Ndoa

Twawachukuwa watu kama wapendwa maumbile wa Mungu. Twachukuwa pia uhusiano (wa ndoa) kama jambo hai ambao huitaji utayarishaji na uleaji.

Jamii yetu ni nene na yenye kupokea watu. Kanisa la Muungano la unga ndoa ya:

  • Watu walio talikiwa
  • Mke na mume wa dini tafauti

Twaamini kwamba Mungu ataka uhusiano wa mapendo uwe wenye uaminifu, wenye heshima, wenye haki, wenye uponyaji, na wenye kudumisha waliounga ndoa na wale wanao kuwa karibu nao.Hii uhusiano inaweza kuwa kati ya mke na mume, ama kati ya watu wa aina moja.

Kwa habari zaidi, tazamaneni “Ndoa na Maisha ya Ushirikiano” (Marriage).

Uhusiano wa imani mbali mbali

Kanisa la Muungano la Kanada lachukuwa desturi ya dini zingine za watu wote na heshima na shukrani. Twaamini kwamba Roho wa Mungu yafanya kazi katika jamii nyingi tafauti za imani.

Kwa wakristu.Yesu ndiye njia kwakumjua Mungu.Ufahamu wetu hauja kadhirishwa na uwezo wa kibinadamu. Ukubwa wa Mungu wa dumu na wafanya kazi katika dunia yetu kwa kupitia roho ambao haitautishi mlango wa kanisa la wakristu, ma buda, baniani, ama hekalu ya ma siki, nyumba ya maabudu ya wakaaji wa kwanza wa Kanada, msikiti ya wasilimu, sunagogi ya wayaudi.

Twafanya kazi pamoja na makanisa mengine za wakristu wakatiwowote iwezekanayo, na katikati watu wa imani zingine inchini Kanada na katika duniani nzima kuhusu mambo ya sheria, amani na heshima ya kibinadamu.

Kwa sasa, tofauti iko popote pembeni yetu,na twaamini kwamba hiyo ni sababu ya kusherekeya.

Haki ya ujamii

Kuwajali wengine ilikuwa moja ya mafundisha muhimu ya Yesu: kuwalisha wenyi njaa, kuwa ridhisha wenyi kiu, kuwajali wagonjwa, kuwavika waliwo tupu, kuwajali wasikwao, kuwatembelea wafungwa.

Twaamini kwamba twawatiya moyo wengeni kufanya kazi, kupitia neema ya Mungu, kwaajili ya Dunia bora. Kwaajili ya hiyo, twashirikiyana na ma kanisa zingine, imani za mila, na watu wenyi ufadhili kwakumaliza umaskini na kuwajalii wasiojiweza.

Katika Afrika, Ezia, Amerika ya Kilatini, na karaibe, Kanisa la Muunguno latumika na ma kanisa pamoja na vikundi143 ambao twawaita washirika . twawasaidiya  katika kazi zao ambazo wazichukuwa kama zamuhimu katika maisha yao. Hii ya tuhusu kuwalisha wenyi njaa, kuwajali wagonjwa, kuwajali wasio na makao zaidi hata zaidi uwezo wetu.

Kwahabari zaidi kuhusu, tafadhali jioneeni, Social Justice.

Last updated:
2007/05/23
Created:
2007/05/23