The United Church of Canada crest /L'Église Unie du Canada
3250 Bloor St. West, Suite 300
Toronto, ON M8X 2Y4 Canada
Toll-Free: 1-800-268-3781
Fax: 416-231-3103
Website: www.united-church.ca
Loading
Quick Links

Overview

Kauli Muhimu za Mafundisho Yetu

Trouble reading this page? See our help page!

Sehemu hii inawasilisha kauli muhimu za kihistoria za mafundisho ya Kanisa la Muungano – hati zinazoelezea kiini cha imani yetu.

Kila wakati, Kanisa la Muungano hutaja tena imani yake katika njia mpya ili kukidhi mazingira yanayobadilika na changamoto mpya. Hivyo, kutaja kiini cha imani yetu ni shughuli inayoendelea.

Kulingana na ufahamu kwamba Biblia ni kiwango cha mwisho cha imani yetu, uanachama katika kanisa umeegemea katika kukiri imani, na sio kufuata kanuni ya imani fulani. Wanachama wapya hutakiwa kukiri imani ya Mungu katika nafsi tatu – Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu – na kujitoa wenyewe kuwa wenye tabia ya uaminifu katika kanisa na duniani. Zaidi ya hapo, wahubiri wa Kanisa la Muungano wanatakiwa kuwa katika “makubaliano ya msingi” na Vifungu 20 vya Imani vilivyo katika “Msingi wa Muungano”.

Mwili Mmoja wa Kristo

Kama viungo vya mwili wa Kristo, tunatambua urithi wetu wa Mageuzo ya Kanisa na mafundisho ya kanuni za imani za kanisa la zamani, hasa ile ya Mitume na ya Nikea.

Uanachama wetu katika Baraza la Makanisa Duniani unatuunganisha sisi na ushirika wa makanisa yanayomkiri Bwana Yesu Kristo kama Mungu na Mwokozi kufuatana na maandiko.

Juu ya yote, tunafuata nyayo za imani yetu kwenye maandiko ya Agano la Kale na Jipya, ambamo ushuhuda wake ni kiwango cha msingi cha imani na maisha.

Kukiri Imani Yetu

Mafundisho ya Kanisa la Muungano la Kanada yameelezwa katika “Msingi wa Muungano”(1925), ambayo yanajumuisha Vifungu 20 vya Imani.

Kanisa lilitaja tena imani yake katika njia mpya katika Kauli ya Imani la mwaka1940. Kauli hii inatukumbusha kwamba “Imani ya Kanisa ni Injili ya upendo mtakatifu na wa wokovu wa Mungu uliofunuliwa na Yesu Kristo”. Pia inatamka kuwa kila kizazi kipya kimeitwa kutamka injili hii kwa upya, “kwa mantiki ya mawazo ya wakati wao na kwa mkazo unaokidhi mahitaji ya wakati wao”.

Wito wa kurejea maungamo yetu ulipelekea kwenye Kanuni Mpya ya Imani (1968), uthibitisho wa imani ulitumika sana katika ibada zetu. Pia ulipelekea kwenye kauli kama vile Ubwana wa Yesu (1978) na Mamlaka na Tafsiri ya Maandiko (1992).

Wakati huu, kanisa linatafiti na kujadili pendekezo la kauli mpya ya imani, Wimbo wa Imani, ambayo itafikiriwa na Baraza Kuu la 39 mwezi Agosti 2006.

Last updated:
2007/05/27
Created:
2007/05/27